Huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya afya wakati wa hedhi miongoni mwa wasichana na wanawake, wito umetolewa kwa wanaume kujitenga na dhana potovu na badala yake wawe katika mstari wa mbele kuhakikisha wasichana na wanawake wanahudumiwa vilivyo wakati wao wa hedhi.
Wito huu umetolewa na Naibu Gavana wa Busia Arthur Odera na MCA wa Chakol kusini Dalmas Onjole, ambao wametoa changamoto kwa wazazi wa kiume kuwapa mazingira salama wanao na wake zao wakati wako kwenye hedhi kwa kuwanunulia vifaa hitajika. "Maswala ya hedhi yasiwe ni siri tena, jamii yote yafaa jumuika kuhakikisha afya ya mtoto wa kike.
Dunguzanguni tupuzilie mbali dhana potovu kwenye swala hili," Naibu gavana Odera alisema.
Washikadau hao wametoa wito kwa serikali kurahisisha namna ya upatikanaji wa taulo za hedhi ili kuhakikisha wasichana wengi ambao hawana uwezo wa kupata sodo hawataabiki wakati wa hedhi.